Homa ya kombe la dunia inazidi kupanda zikiwa zimebaki takribani wiki
zipatazo nne kabla ya michuano hiyo haijaanza kutimua vumbi kwenye
viwanja tofauti nchini Brazil. Timu zote 32 tayari zimeshatangaza vikosi
vyao kwa ajili ya michuano hiyo.
Katika vikosi vyote vya timu za taifa vilivyotajwa kwa ajili ya kombe
la dunia Brazil 2014 – Klabu ya Bayern Munich ndio inaoongoza kwa kutoa
wachezaji wengi – imetoa wachezaji 17 watakaowakilisha mataifa
mbalimbali kwenye kombe la dunia.
Klabu ya Manchester United inashika nafasi ya pili baada ya Bayern na
nafasi ya kwanza EPL kwa kutoa wachezaji wengi walioitwa kwenye timu za
taifa zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia – UNITED imetoa
wachezaji 16.
Chelsea ya England imeshika nafasi ya 3 kwa kutoa wachezaji 15,
Napoli 14, Barcelona na Real Madrid wametoa wachezaji 13 kila timu,
Juventus imetoa wachezaji 13.
0 comments :
Post a Comment