Friday 11 October 2013

MWANAMKE HUYU APEWA TALAKA KWA KUMBUSU FARASI..


Mwanaume mmoja nchini Saudi Arabia amempa Talaka mpenzi wake kwa kumbusu farasi..Mwanaume huyo
aliziona picha hizo za mke wake katika mtandao mmoja wa kijamii  akimpa bonge la busu farasi huyo katika shamba moja karibu na Riyadh..
Mwanamke huyo hakushtushwa na kitendo hicho cha mumewe kumpa talaka kwa kumbusu Farasi..
Gazeti moja nchini humo limeripoti kua mwanamke huyo hakujutia kitendo alichokifanya na aliongezea kuwa hakushangazwa kuachana na mwanaume ambaye hawezi kutofautisha mnyama na binadam.
Alisema pia anajisikia furaha kupiga hizo picha maana zinaonyesha upendo wake kwa farasi nchini humo..

0 comments :

Post a Comment